HaSwa Digital Logo

HaSwa Digital

Teknolojia kwa Elimu na Maendeleo

Kuhusu Sisi

HaSwa Digital ni taasisi ya teknolojia inayolenga kutumia TEHAMA kama nyenzo ya kukuza elimu, ubunifu, na maendeleo ya jamii. Tunajikita katika kuandaa na kusambaza suluhisho za kidijitali zinazowasaidia wanafunzi, taasisi, na jamii kwa ujumla kuendana na kasi ya sayansi na teknolojia.

Dira Yetu

Kuwa kinara wa matumizi ya teknolojia katika kuimarisha elimu na maendeleo ya kijamii nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Dhamira Yetu

Kuwezesha vijana, wanafunzi, na taasisi kwa kuwapatia maarifa ya kidijitali, rasilimali za teknolojia, na mazingira ya kujifunzia yanayochochea ubunifu, utafiti, na maendeleo endelevu.

Malengo Yetu

Kuhusu Mwanzilishi

Hamisi Salehe Mohamedy ni mwanzilishi wa HaSwa Digital na mtetezi wa matumizi ya teknolojia katika elimu na maendeleo ya jamii. Anaamini kuwa kuwapatia wanafunzi fursa ya mapema ya teknolojia ni msingi muhimu wa kujenga kizazi chenye ujuzi, ubunifu, na ushindani wa kimataifa.